Ajali yauwa 12 na wengine 46 wajeruhiwa

Basi la kampuni ya mabasi ya CITY BOYS lililokuwa linatoka Karagwe mkoani Kagera kwenda jijini Dar es salaam, hapo jana majira ya usiku limeripotiwa kupata ajali maeneo ya Makomero wilayani Igunda mkoani Tabora.
Jumla ya watu kumi na mbili (12) walipoteza maisha, ambapo watu kumi (10) walifariki papo hapo eneo la tukio huku wawili (02) wwalifariki wakiwa njiani, wakikimbizwa kupelekwa katika hospitali ya wilaya Igunga kwa ajili ya matibabu. Jumla ya majeruhi arobaini na sita (46) wamefikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Aidha, kati yao watu watatu (03) walikuwa na hali mbaya sana (mahututi), ambapo wanaume ni wawili(02) na tayari wamepelekwa hospitali ya Bugando iliyoko jijini Mwanza na mmoja mwanamke alipelekwa hospitali ya Nkinga usiku wa kuamkia leo.
Kaimu RTO mkoa Tabora, inspekta Hardson amethibitisha kutokea ajali hiyo iliyotokea aprili 04 2018 majira ya usiku. Ajali ilihusisha gari lenye namba T486 ARB aina ya Fuso la mizigo na basi la abiria lenye namba T983 DCE aina ya Scania la kampuni ya mabasi ya City Boys.
Kamanda wa polisi Hardson amesema gari aina ya Fuso iliyokuwa imebeba mzigo wa viazi ikitokea mkoani Singida kuelekea wilaya Igunga, ghalfa tairi yake upande wa kulia ilitumbukia katika mashimo mawili yaliyopo barabarani iliyopelekea tairi kupasuka na ream kupinda, na kupelekea mfumo wa usukani kukatika katika maungio ya starring rod na starring box, kisha gari kukosa muelekeo na kusababisha ajali kwa kuligonga basi la abiria la mabasi ya City Boy.
“Dereva wa basi amekufa papo hapo na wahusika wa Fuso kwa taarifa za awali wamekimbia baada ya ajali hii.” Alisema Hardson kaimu RTO mkoani Tabora.
Ajali yauwa 12 na wengine 46 wajeruhiwa Ajali yauwa 12 na wengine 46 wajeruhiwa Reviewed by KUSAGANEWS on April 05, 2018 Rating: 5

No comments: