Ester Bulaya Aitwa Polisi

Mbunge wa Bunda Mjini kupitia CHADEMA Ester Amos Bulaya, ameitwa kituo cha polisi cha kati jijini Dar es salaam huku akiwa hana taarifa za sababu ya wito huo
Akizungumza Ester Bulaya amesema amepata taarifa za kuitwa kwake polisi kutoka kwa mwanasheria wake na hivi sasa yuko njiani kuelekea kituoni hapo, ingawa hajui kitakachomkuta huko.
“Ni kweli nimepata taarifa kutoka kwa mwanasheria wangu, naitwa kituo cha Polisi na sasa hivi ndio nalekea huko central, sababu za wito huo sijui lakini huenda ikawa kama ya wenzangu kina Mdee”, amesema Ester Bulaya
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kuwakamata viongozi na wabunge wa CHADEMA na kuwafungulia mashtaka, ambayo baadhi yao wengine wameshapandishwa mahakamani, kwa mashtaka ya kufanya maandamano bila kibali na kusababisha vurugu.
Ester Bulaya Aitwa Polisi Ester Bulaya Aitwa Polisi Reviewed by KUSAGANEWS on April 05, 2018 Rating: 5

No comments: