Rais John Magufuli amefanya mazungumzo na kamishna wa amani na
usalama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Balozi Smail Chergui aliyewasilisha
ujumbe wa mwenyekiti wa kamisheni hiyo, Moussa Faki Mahamat
Chergui amesema leo Aprili 20, 2018 katika mazungumzo na Rais
Magufuli yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
Taarifa ya Ikulu imesema viongozi hao wawili wamejadili masuala
ya amani na usalama barani Afrika na hasa ukanda wa maziwa makuu
Amesema pia wamejadili masuala ya wakimbizi, huku akimshukuru
Rais Magufuli kwa ushauri, mchango wa mawazo na uzoefu katika kuimarisha
amani na usalama
Wakati huohuo , Rais Magufuli amekutana na msaidizi wa Rais wa Misri na waziri
mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Ibrahim Roshdy Mahlab aliyewasilisha ujumbe kutoka
kwa Rais wa Taifa hilo, Abdel Fattah el-Sisi
Baada ya mazungumzo, Mahlab amesema wamejadili namna ya
kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Misri, ikizingatiwa
kuwa zipo fursa nyingi ambazo nchi hizi mbili rafiki zinapaswa kuzifanyia
kazi
Mahlab amebainisha kuwa utekelezaji wa makubaliano yaliyowekwa
wakati wa ziara ya Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi nchini umeanza ambapo
tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi imeshakutana nchi Misri na
kuainisha maeneo yenye fursa na yanayopaswa kufanyiwa kazi.
|
Magufuli apokea ujumbe wa kamisheni ya amani AU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment