Sababu za bajeti Wizara ya Afya kupungua


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 imepungua kwa asilimia 19.6 ikilinganishwa na ya 2017/18 kutokana na dhamira ya Serikali kutumia fedha za ndani kuitekeleza

Akijibu hoja zilizoibuka wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, Ummy alisema mwaka jana wabunge waliishauri Serikali kupunguza utegemezi kutoka wa wafadhili katika kutekeleza bajeti ya afya

Bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19 ni Sh898.3 bilioni tofauti na mwaka 2017/18 unaoishia Juni ya Sh1.07 trilioni

“Waheshimiwa wabunge, mwaka jana wakati nawasilisha bajeti hapa mlieleza wazi kwamba bajeti inategemea wafadhili. Kilichotokea bajeti Wizara ya Afya kwa mwaka huu fedha za ndani zimeongezeka kutoka Sh628 bilioni hadi Sh681 bilioni lakini fedha kutoka kwa wafadhili zimeshuka,” alisema Ummy

“Hii imeonyesha dhamira ya Rais John Magufuli kutaka kupunguza utegemezi wa wadau wa maendeleo katika kupunguza changamoto za Watanzania.”

Alisema lengo ni nchi kuanza kujipima yenyewe katika utekelezaji wa bajeti ili kuona ni kwa namna gani inaweza kutatua changamoto zilizopo

Juzi, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilieleza kuwa bajeti ya wizara hiyo imepungua kwa asilimia 19.6 na kwamba kutaleta athari katika utoaji wa huduma kwa wananchi

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alisema katika bajeti ya mwaka 2017/18, fungu la fedha za maendeleo, wizara ilitengewa Sh785 bilioni na hadi kufikia Februari Sh385.77 bilioni, kiasi ambacho ni sawa na asilimia 49 kilipokewa na ili kutekeleza miradi

Alibainisha kuwa kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh336.3 bilioni ni za kutoka vyanzo vya ndani na Sh449.5 bilioni kutoka vyanzo vya nje

“Kamati imebaini fedha zilizopokewa kutoka vyanzo vya ndani ni Sh64.7 bilioni sawa na asilimia 19 ya fedha zilizoidhinishwa. Fedha za nje zilizopokewa ni Sh321 bilioni sawa na asilimia 71,” alisema.

Sababu za bajeti Wizara ya Afya kupungua Sababu za bajeti Wizara ya Afya kupungua Reviewed by KUSAGANEWS on April 20, 2018 Rating: 5

No comments: