Mkazi mmoja mkoani
Kigoma aliyejulikana kwa jina la Ndimugwanko Mlovezi anashikiliwa na Jeshi la
Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga mkewe na kumuua.
Akizungumza tukio hilo Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Ottieno, amesema tukio hilo limetokea April 20
ambapo mwanaume huyo alimpiga mkewe Bi. Selina Simon hadi kumuua, akimtuhumu
kwa nini anamzalia watoto wa kike pekee.
“Tukio limetokea tarehe 20 April saa
moja na nusu jioni katika kijiji cha Itundiko, Kakonko, mama aniatwa Selina
Simon mwenye miaka 35, aliuawa kwa kupigwa na mume wake Ndimugwanko Mlovezi
mkazi wa kijiiji hicho hicho kwa kumpiga na fimbo maeneo mbali mbali ya mwili
wake, chanzo kikubwa kilichopeleka kipigo hiko kulikuwa na ubishano mkubwa kati
ya marehemu na mtuhumiwa, juu ya kumzalia watoto wa kike mfululizo bila
kumzalia wa kiume,ndio chanzo cha kumpiga", amesema Kamanda Ottieno.
Kamanda Ottieno amesema mtuhumiwa
huyo atafikishwa mahakamni hapo kesho April 24 kujibu mashtaka yake
yanayomkabili.
Kigoma, amuuwa mkewe kisa kumzalia watoto wakike
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment