Mmiliki wa Shule ya Sekondary ya St. Patrick
ya jijini Dar es Salaam, Ndele Mwaselela amejitolea kumsomesha mtoto wa
marehemu Agnes Masogange, Sania(11) kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na
akifaulu hadi chuo kikuu
Hii ni neema nyingine kwa mtoto huyo wa
pekee wa Masogange aliyemuacha, baada ya jana kamati ya maandalizi ya mazishi
kupitia mweka hazina wake, Zamaradi Mketema kueleza kuwa wamemwekea Sh2 milioni
zilizobaki katika michango ya msiba huo kwenye akaunti yake
Zamaradi amesema fedha hizo zimewekwa
mahususi kwa ajili ya kumsaidia kianzio katika cha ada atakapoanza kidato cha
kwanza mwakani kwa kuwa mwaka huu anatarajiwa kumaliza darasa la saba
Akizungumza leo Jumatatu Aprili, 23 katika
shughuli za mazishi,
zilizofanyika nyumbani kwa baba wa Masogange, Kijiji cha
Utengule, Wilaya ya Mbalizi, Mwalesela amesema mbali ya kumsomesha pia mtoto
huyo atakaa hosteli kwa gharama zake kwa muda wote wa masomo yake
“Akifaulu kidato cha nne pia atasomeshwa na
mimi hadi kidato cha tano na sita lakini pia akifaulu atakwenda hadi chuo
kikuu,” |amesema
Kutokana na maamuzi hayo, alimtaka msanii
Irene Uwoya ambaye mtoto wake naye anasoma katika shule hiyo, kuhakikisha
anapokwenda kumsalimia mwanaye awe anakwenda kumsalimia na Sania
“Hivyo wewe msanii Uwoya una mtoto wako
pale shuleni kwangu naomba ukija kumuona hakikisha unamuona na mtoto huyo,”
amesema Mwaselela
Ajitolea kumsomesha mtoto wa Masogange hadi chuo kikuu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment