Wema akutwa na hatia mahakamani


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakzi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, na kusema kwamba Wema na Wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la, na ndipo Hakimu Simba akasema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea, na ndipo aliposema baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo, imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Wema na wafanyakazi wake wawili wanakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bhangi, na kesi hiyo imehairishwa mpaka Mei 14 mwaka huu.

Wema akutwa na hatia mahakamani Wema akutwa na hatia mahakamani   Reviewed by KUSAGANEWS on April 23, 2018 Rating: 5

No comments: