Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka jeshi la polisi
kufanya lolote lililopo ndani ya uwezo wao, ili kuhakikisha mani ya nchi
haivunjwi na kubaki na utulivu.
Kauli hiiyo imetolewa leo jijini
Arusha alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, na kusema
kwamba anatambua kazi ya jeshi la polisi ingawa kuna watu ambao wana wabeza, hivyo
wasiyumbishwe na watu hao, ila waendelee kuchapa kazi kwani yeye kama Amiri
Jeshi Mkuu wao yuko pamoja nao.
“Kuna watanzania wanaongea
maneno ya kebehi kebehi kuhusu polisi, hawajui thamani ya polisi, ndugu zangu
polisi tembeeni kifua mbele, na kwa bahati nzuri mimi ni shemeji yenu, mkwe
wenu, msiwe na wasi wasi, maneno ya kashfa na kebehi yanayozungumzwa na wengine
wala yasiwakatishe tamaa. Nilipopewa urais nikaapa kuhakikisha nchi inakuwa
salama, na kuhakikisha nchi inakuwa salama, lazima jeshi la polisi liwe salama,
endeleeni kuilinda amani ya nchi yetu, mtakayoyaamua yaamueni na mimi
nitawasapoti, niliapa kuilinda amani ya nchi hii kwa nguvu zote na nitailinda”,
amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hilo Rais Magufuli
amesema anatambua mazingira magumu waliyonayo askari polisi hususan wa vyeo vya
chini, hivyo atahakikisha anatatua kero zao ikiwemo kuboresha makazi yao.
Jeshi la Polisi wapewa Kufanya Lolote lililopo ndani ya Uwezo wao.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment