Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapiga marufuku askari polisi
kufyeka mashamba ya bhangi, kwani hiyo siyo kazi walioajiriwa kuifanya.
Rais Magufuli ametoa marufuku hiyo
leo alipokuwa akihutubia wananchi waliofika kwenye sherehe za uzinduzi wa
nyumba za askari polisi mkoani Arusha, zilizofanyika uwanja wa Sheikh
Amri Abeid, na kusema kwamba jambo hilo sio kazi yao.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema
kwamba kazi ya kufyeka mashamba ya bhangi ni ya wenyewe wananchi wanaolima
bhangi hizo, na iwapo hawatamkamata mhusika wa shamba, basi wasombe kijiji
kizima kwenda kulifyeka.
“Ninyi hamkuajiriwa kwenda kufyeka
mashamba ya bhangi, makamanda wako na maaskari wako, wasikate mashamba ya
bangi, hawakuajiriwa kufyeka bhangi, tumieni njia za intelijensia wenu
mtamshika tu, kama shamba lipo karibu na kijiji, shika kijiji kizima, wazee,
wanawake, watoto, ndio wakafyeke hilo shamba la bhangi, ila IGP usiwatume
maaskari wako kufyeka bhangi, mtaumwa nyoka mle, mna uniform nzuri
msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bhangi, mimi nisingefyeka bhangi, wa kufyeka
wapo”, amesema rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema
kwamba kazi yao ni kuhakikisha nchi inakuwa salama, hivyo masuala kama hayo sio
majukumu yao pia ni udhalilishaji kwa jeshi la polisi.
Polisi wapigwa marufuku kufyeka mashamba ya bhangi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment