Jeshi la Polisi Kitengo
cha usalama Barabarani, Mkoani Mbeya limewafutia leseni Madereva watano wa
Magari ya abiria baada ya kubainika wamekiuka sheria za usafirishaji.
Akizungumza Mkuu wa Polisi
Kitengo Cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Leopard Fungu amesema kume kuwepo
na wimbi kubwa la ajali ambazo zimegharimu maisha ya watu wengi zinatokana na
uzembe wa baadhi ya madereva kwa kutoheshimu sheria za usafirishaji.
"Katika kipindi hiki cha wiki tatu
nimewafungia takribani madereva watano leseni zao. Tumechukua hivyo kutokana na
hatutaki mchezo barabarani",
amesema Leopard.
Kwa upande wake Afisa mfawidhi
Sumatra kanda ya Mbeya, Denis Daudi amesema katika kudhibiti wimbi la ajali
mkoani Mbeya, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na majini Sumatra wameeleza kuwa
katika oparasheni wanayoendelea nayo wamebaini makosa kadhaa kwenye magari na
kuchukua hatua stahiki dhidi yao.
Jeshi la Polisi lawachukulia hatua kali madereva
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment