Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, George Mkuchika amesema kazi kubwa ya usalama wa taifa ni
kukusanya habari na kuishauri serikali na wala si kukamata watu kwa mabavu
Mkuchika ameyasema hayo leo Aprili 16
bungeni wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha
makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019
“Naomba nichukue nafasi hii kufafanua sheria
ya usalama wa taifa inasema nini, usipojua kazi za idara ya usalama wa taifa,
utawapa lawama kwa kazi ambazo si zao,” amesema
Amesema idara hii hutekeleza majukumu
kulingana na sheria ya usalama wa taifa namba 15 ya mwaka 1996 na sheria hiyo
katika kifungu cha nne, inasema kazi yake ni kukusanya, kuchambua na kuishauri
serikali hatua za kuchukua
Amesema ameamua kulisema hilo kwa kuwa
wabunge wengi wamezungumzia kuhusu watu wa idara ya usalama kukamata watu ovyo
na kwa kutumia mabavu
“Pili haitakuwa kazi ya idara ya usalama,
kumfuatilia fuatilia mhalifu. Nimeona niiseme hiyo kwa sababu mazungumzo mengi
yameelekeza huko, mtu ameuawa ni ‘polisi kesi’, hakuna nchi ambayo idara ya
usalama ina shughuli ya kukamata watu,” amesema
Amesema: “Kama mnataka usalama wa
taifa wafanye kazi ya kukamata watu basi walilete suala hilo bungeni.”
Mkuchika aeleza majukumu ya usalama wa taifa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment