Wananchi wa kijiji cha Butahyaibega Wilaya
ya Bukoba wameendesha msako usiku kucha wakimtafuta mtuhumiwa wa mauaji ya
watoto wake pacha
Mtuhumiwa huyo, anadaiwa kuwaua kwa
kuwachinja pacha hao, usiku wa kuamkia siku ya Jumapili
Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Bulambizi,Dickson Barongo amesema usiku kucha wamekesha wakiendesha msako
maeneo yote ya kijiji na kufanya ukaguzi maporini wakimsaka mtuhumiwa
"Tumezingira maeneo yote yanayoingia na
kutoka kwenye kijiji msako umefanyika usiku kucha wananchi wameungana kwa
pamoja kumtafuta mtuhumiwa mpaka atakapopatikana tuna uhakika hajatoka nje ya
kijiji cha Butahyaibega,"amesema Barongo
Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni ugomvi wa
kifamilia
Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Kagera,
Isaac Msengi amesema ufafanuzi wa suala la mauaji hayo utafanywa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi
Wanakijiji wafanya msako
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 16, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment