Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amemaliza muda wake wa majukumu ya
tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kilichoanzia Aprili 30,2 013 hadi Aprili
29, 2018 ambapo yeye na wajumbe wa tume hiyo wamekabidhi ripoti yao ya kazi.
Akitoa taarifa yake kwa Rais wa
ZanzibarDkt. Ali Mohamed Shein, Jecha amesema kuwa tume inaamini kwamba,
mafanikio yaliyopatikana wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hasa ya kiuchaguzi
yalitokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali na wananchi kwa jumla.
"Ndani ya miaka mitano tume
imeweza kuendesha jumla ya chaguzi ndogo nne, zikiwemo chaguzi ndogo tatu za
Udiwani na chaguzi moja ya uwakilishi pamoja na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Oktoba
25,2015 na ule wa marudio yake Machi 20, 2016. Tume imefanya mapitio ya majimbo
ya uchaguzi na kubadilisha mipaka ya majimbo ya uchaguzi, majina ya majimbo na
kuongeza idadi ya majimbo kutoka 50 hadi 54", ameeleza Jecha.
Pamoja na hayo, Jecha ameendelea kwa
kusema "Tume imeweza kufanya uandikishaji wa wapiga kura kwa
awamu mbili na kuliendeleza daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na
kuendesha programu mbalimbali za elimu ya wapiga kura kupitia vyombo vya
habari, mikutano ya wadau, uchapishaji wa vipeperushi, majarida na makala
mbalimbali".
Aidha, Mwenyekiti huyo amemueleza
Dkt. Shein kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imechaguliwa kuwa kiongozi wa
Uchaguzi Mkuu wa nchini Congo utakaofanyika mwezi Disemba mwaka huu.
Kwa upande wake, Rais wa
Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein ameipongeza Tume hiyo kwa kutekeleza vyema
majukumu yake ndani ya miaka mitano kwa kuendesha chaguzi zote .
"Tume hii inastahiki
pongezi kwa kuifanikisha vyema kazi waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuendesha
chaguzi zote ukiwemo uchaguzi Mkuu, chaguzi ndogo na ule uchaguzi wa marudio
ambazo zote hizo zilifanywa kwa ufanisi mkubwa", amesema Dkt. Shein.
Wajumbe wa tume hiyo ambao
wamemaliza muda wao ni Mwenyekiti mwenyewe Jecha Salim Jecha, Jaji Abdul-hakim
Ameir Issa, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari
Hamad, Haji Ramadhan Haji na Salmin Senga Salmin ambao wote hao waliapishwa
rasmi Mei,4, 2013.
Jecha ang'atuka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment