Mwenyekiti wa CHADEMA
Taifa, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe leo
April 17 amezuiwa na maafisa wa jeshi la polisi kuongea na waandishi wa habari
baada ya kutoka mahakamani katika kesi yao inayowakabili ya kufanya maandamano
yaliyopelekea kifo cha Akwelina.
Baada ya Mbowe na viongozi wengine
waandamizi wa CHADEMA kutoka mahakamani waandishi wa habari walijotokeza na
kutaka
kufahamu kilichojiri na kupata
maelezo yoyote kutoka kwa viongozi hao lakini alijitokea afisa mmoja wa jeshi
la polisi na kuwazuia viongozi hao wasifanye mazungumzo na waandishi wa habari katika
viunga hivyo vya mahakama kwa kudai kuwa hawapaswi kufanya hivyo.
Jambo hilo lilileta mvutano wa
maneno katika ya viongozi hao wa CHADEMA pamoja na Afisa huyo wa polisi, lakini
baadae Mwenyekiti wa CHADEMA aliaanza kuondoka akielekea kwenye gari yake hapo
ndipo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza waandishi wa habari kuwa jeshi la polisi
halitaki wao waongee na waandishi pamoja na Umma kiujumla.
"Tunapotoka lazima tutoe
statement kwa vyombo vya habari sasa unataka tukafanyie barabarani au
tukatafute ukumbi, nyinyi mna abuse power ambayo unapewa na state, yaani
mnapitiliza . Jamani inabidi tuachie hapo tu maana mnaona wamekataa
tusizungumze na sisi hatutazungumza lakini haki itabakia haki, hatujawahi kuona
watanzania wanazuiwa kuzungumza na watanzania wenzao kuwapasha habari.
Walitukamata na kutuleta kwenye mashtaka hiyo yenyewe ni habari saizi
wanakataza hata tusizungumze hili jambo la ajabu sana ni matumizi mabaya ya
madaraka na polisi wakiendelea na mtindo huu wataleta vurugu zisizo na sababu
katika nchi ahsanteni sana" alisisitiza
Mbowe
Freeman Mbowe azuiwa mahakamani na maafisa wa Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment