Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi
wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka
2015 hadi Machi mwaka huu
Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 7 na Mkuu wa
Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John
Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha
Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha
Sirro amesema kazi ya Jeshi la Polisi ni
kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi
wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza
Amefafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana
askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na
kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi
Amesema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari
165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14
“Hatuna muhali kuwachukulia hatua askari
wanaokiuka utaratibu na nidhamu ya utendaji katika Jeshi la Polisi,” amesema
IGP Sirro
IGP Sirro jumla ya askari 458 walifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment