Mbunge wa Kawe kupitia
CHADEMA Halima James Mdee, amesema kwamba shirika la ndege la Tanzania (ATCL )
halikujipanga kufanya biashara, licha ya kwamba serikali imeshapoteza fedha
nyingi na inaendelea kupoteza zaidi kuwekeza kwenye shirika hilo.
Akizungumza Bungeni Halima Mdee
amesema kutokana na ripoti iliyotolewa na wenyewe ATCL imesema kampuni hiyo
ilikuwa haina mpango wa biashara, lakini serikali imekuwa aikilipa kipaumbele
kuendelea kuwekeza pesa, licha ya changamoto nyingi inazopitia ikiwemo na
ukosefu wa wataalam.
“Naomba nije suala la kitaifa
la ATCL, tunaambiwa kwamba kwa mwaka hu wa fedha serikali inatarajia kununua
ndege mpya, hoja sio kupinga ununuzi wa ndege, hoja ni hizi fedha matrilioni ya
shilingi, zinaenda kuzalisha au tunaenda kuzitupa chini na zinapotea . Nina
taarifa ya msajili wa hazina, ndio amepewa dhamana ya kusimamia mashirika yote
Tanzania, anasema kwamba imekuwa vigumu kwa ofisi yangu kufanya uchambuzi wa
kina wa utendaji wa ATCL kutokana na kutokuwepo taarifa za kutosha kuhusu
kampuni", amesema Halima Mdeee.
Halima Mdee ameendelea kwa kusema
kwamba ...”ukija kwenye taarifa yenyewe ya ATCL inasema shirika halikuwa
na mpango wa biashara, mwaka 2018/19 tunataka tuwekeze bilioni 495 halafu
hatuna mpango wa biashara, unaanzaje bishara halafu hakuna mpango!? Shirika lina
madeni Mwenyekiti, shirika halina mpango wa biashara, shirika halina wataalamu,
tunaweka trilioni 1”.
Kutokana na hilo Halima Mdee
ameitaka serikali kuwa makini kwenye suala la kuwekeza kwenye ATCL, kwani
wakigundua wamefanya kinyume na inavyotakiwa itawawajibisha.
Halima Mdee 'alipuka' na ATCL Bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment