Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo amefunguka na kuwashauri wanaume wenzake kuacha tabia za
kuwanyanyasa wake zao pindi wanapokuwa majumbani mwao kwa kuwafanyia vitimbi
mbalimbali bila ya kufikilia kuwa mafanikio aliyokuwa nayo yametokana na mwenza
wake huyo kwa namna moja ama nyingine.
Gambo ametoa nasaha hiyo kupitia
ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo rundo la wanaume wenye
chembechembe za tabia ya kuwaona si kitu wake zao pindi wanapokuwa wamepata
mafanikio ya kimaisha na kusahau kuwa walianza pamoja harakati za kuomba Mungu
awape mafanikio ya kimaisha.
"Familia nyingi zipo kwenye
mateso makubwa sana kutokana na matendo ya wanaume ndani ya nyumba. Mwanamke
mnaanza naye maisha, mnateseka naye mkiwa hamna chochote halafu Mungu anakupa
riziki unaamua kumtesa mkeo. Wakati mwingine mwanaume unachukua hata chakula
cha ndani (unga , mchele, sukari na nk) alichokihangaikia mkeo kwa ajili ya
watoto wake na kupeleka nyumba ndogo", amesema Gambo.
Pamoja na hayo, Gambo ameendelea kwa
kusema "nadhani haya mambo ni sababu kubwa za presha na sukari
kwa familia nyingi. Wanaume ni busara kuheshimu nyumba yako hata kama una
vituko vyako".
Kwa upande mwingine, Gambo amesema
kuna hitajika tiba mbadala ya kuzisaidia familia zenye matatizo hayo kama taifa
ili mradi kuweza kuwa wasaidizi wanawake waliolewa na wanaume wenye kadhia hiyo
ambayo haipendezi mbele ya jamii wala kwa Mungu.
"Familia nyingi zipo kwenye mateso"- Gambo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment