Mbunge wa Vunjo kupitia
NCCR – Mageuzi James Mbatia, amesema suala la upotevu wa trilioni 1.5 kwenye
ripoti ya CAG sio jambo dogo bali ni janga la kitaifa, kwani fedha hiyo
ingeweza kufanya mambo makubwa kwa wananchi wake, ikiwemo ujenzi wa barabara.
Akizungumza Bungeni leo Mheshimiwa
Mbatia amesema kuna matukio mengi yanayotokea nchini lakini hayapatiwi
ufumbuzi, ikiwemo miradi mibovu inayoteketeza pesa za umma ambazo zingeweza
kufanya shughuli za maendeleo, lakini masuala hayo yamekuwa hayafanyiwi muendelezo
au kupata muafaka wake.
"Leo hii Jangwani maji
yaliyofurika pale, mafuriko yaliyotokea juzi, mradi uliotekelezwa pale, nguvu
iliyowekezwa pale, investment iliyowekezwa pale nani anawajibika kwa kushauri
ujinga huo wa depo ya Dar es salaam Rapid Transport !? Ukisoma ile taarifa ya
CAG hili ni janga la kitaifa la 1.5 trilioni, hii ni kashfa juu ya kashfa,
hakuna muendelezo, ule mradi wa kutoka DSM mpaka Bagamoyo boat kashfa, hii
kashfa, ATCL kashfa nyingine”, amesema
James Mabtia.
James Mbatia ameendelea kwa kuitaka
serikali kukubali mawazo ya watu tofauti tofauti katika utekelezaji wa miradi
mbali mbali na masuala mengine, ili kujiepusha na lawama kama hizo.
“Lazima kukubali mawazo
mbadala, tushirikiane vizuri, tufanye kazi vizuri, kwa kuwa Tanzania ni yetu
sote, tusipofuata katiba, tusipofuata sheria, Bunge likajua fasi yake,
kuangalia kodi za Watanzania kama zinatumika vizuri, la sivyo Bunge hili
litakuja kuhukumiwa kwa nini haya yanatokea”,amesema James Mbatia.
Trilioni 1.5 ni janga la kitaifa – James Mbatia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment