Leo ninawaletea makala fupi yenye lengo la kukufahamisha wewe Mtanzania namna mbinu chafu za Wamagharibi( Marekani & Ulaya) zinavyotumika katika nchi nyingi za Afrika, Latini Amerika na Asia kuangusha Utawala uendao kinyume na matakwa yao.
Nchi za Marekani na Ulaya kwa asili yao ni nchi za Kibepari na msingi mkuu wa Ubepari ni unyonyaji katika kile kiitwacho mwenye nguvu na apate ( Suvival for the Fittest ).
Kutokana na msingi huo mkuu wa Ubepari Mataifa haya hufanya kila mbinu kuhakikisha Nchi za Afrika, Asia na Latini Amerika kuwa na viongozi wanaowanyeyekea na wenye ulimbukeni wa Ulaya na Amerika ya Marekani ili iwe rahisi kuwalaghai na Unyonyaji uendelee kutamalaki na kuota mizizi zaidi.
Inapotokea Nchi imempata kiongozi ambaye kwa namna yoyote, matendo yake, kauli zake na hulka yake haiendani na matakwa yao yaani anakuwa kizuizi kati ya Taifa hilo na malengo ya Maperari ambayo ni Unyonyaji, Nchi hiyo aidha ya Latini Amerika, Asia ama Afrika hujikuta katika wakati mgumu kuendesha utawala wake kwa maana Mabepari huanza kutumia mbinu mbali mbali kuuangusha utawala huo thabiti.
Hakika nasikitika kuona Tanzania tumeingia rasmi kwenye Mgogoro huo na Wamagharibi lakini zaidi nasikitika kuona baadhi ya Watanzania wakiungana nao kwa wengi kutokukujua na wachache kwa kujua kutokana na maslahi binafsi kwanza.
Tanzania kupitia uongozi huu wa Awamu ya Tano umejinasibu kwa vitendo, hulka na maneno kuwa haukubaliani na Unyonyaji wa aina yoyote kwa Taifa letu kwa kufanya mambo kadhaa.
Kwanza, ni kufuta Safari zote za nje zisizo na tija kwa Watanzania ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zikifanywa na viongozi wa Serikali, Bunge na Mahakama na hii ilikuwa inatumika kama njia mojawapo ya kuwashawishi viongozi hao kukubaliana na matakwa mbalimbali wakiwa huko ughaibuni kwa maana ni rahisi zidi kumshawishi mtu akiwa nyumbani kwako kuliko akiwa nyumbani kwake. Hii kwa kiasi kikubwa imewanyima fursa nyeti Mabepari ya kukutana mara kwa mara na viongozi wenye dhamana ya maamuzi hapa Tanzania.
Pili, ni namna Serikali ya awamu ya tano inavyoshughulika na wala rushwa na inavyopambana kukemea na kutokomeza ufisadi.
Kiukweli hakuna Taifa lolote la Magharibi linalotamani Tanzania tuwe ni moja ya mifano bora katika jambo lolote kwa kuwa wanatambua kwa sisi kuwa bora katika kupambana na rushwa itakuwa ndio njia ya sisi kupiga hatua za kimaendeleo na kuondokana na umasikini kwa sababu umasikini kwa kiasi kikubwa hutokana na ubadhirifu wa mali za umma ( Ufisadi & Rushwa ), wakati mpango wa "Siri" wa Mataifa ya Magharibi ni kuhakikisha kwa namna yoyote Nchi za Afrika, Latini Amerika na Asia zinaendelea kubaki masikini ili kufanya kuwa jalala la bidhaa duni na mifano mibaya kwa Wananchi wao.
Tatu, Ujenzi wa miundombinu ya reli ya kisasa, usafiri wa anga na mtandao thabiti wa barabara Nchi nzima.
Wamagaribi wanatambua matokea ya kuimarisha njia kuu za usafiri na pia wanatambua ni kwa jinsi gani wao wamepiga hatua kubwa kutokana na mchango wa njia za usafirishaji. Hiki kinachofanyika leo hapa Tanzania hakiwapendezi kwa maana sheria yao na msimamo wao mkuu ni kwamba " Don't Ignore the light smoke as may turn to a big fire", hivyo msimamo wao ni kuzima kila chembe ya moshi wauonao na Tanzania ni miongoni.
Nne, ni kubadilisha sheria za madini. Hii haijawahi tokea katika mataifa mengi ya Afrika, Asia na Latini Amerika ila Tanzania imetokea katika Serikali hii ya awamu ya Tano. Si jambo la kawaida kukemea kwa sauti kuwa "Nyie ni Wezi" na tunataka usawa katika nchi yetu na kila kipatikanacho katika ardhi ya Tanzania ni mali yetu na tunahaki ya kugawana sawa.
Hakika hiki si kitu cha kawaida na mpaka sasa Wamagharibi wanaendelea na mkakati madhubuti wa kulipiza kwa madai ya kuwadhalilisha kwa kuwakemea hadharini kwa kuwa hawajazoea kuambiwa ukweli kutokana na ukubwa waliojijengea na kuwajaza hofu watawala wa Mataifa mengi ya Dunia ya Tatu.
Kutokana na mwenendo huo wa Tanzania kimataifa, ni lazima sisi Watanzania tujiandae kukabiliana na mbinu chafu za kutugawa ambazo zimewezekana katika Mataifa mbalimbali.
Kuna njia kuu tano zinazoweza kutumika kutugombanisha na kutufanya tuingie katika mapambano ya wenyewe kwa wenyewe.
Moja, ni kuunga mkono Chama Kikuu cha Upinzani na kukipatia uwezo wa kifedha ili kukabiliana na Chama tawala. Hii hufanyika kwa kukipa fedha kwa masharti kuwa endapo watafanikiwa kuangusha utawala watashirikishwa kuunda Serikali kwa mujibu ya matakwa yao. Imefanyika hivo katika mataifa mengi ya Latini Amerika mfano South Vietinam mwaka 1963 ambapo kundi dogo la upinzani lilipatiwa fedha na kulaghai Wavietnam hususani vijana, Pia ilitokea hivo hivo Brazili na Guatemala. Sisemi wamefanya hivo ila ni lazima kama Watanzania tuwe makini kufuatilia mienendo ya Vyama vya Siasa katika kipindi hichi tunapokabiliana na mapambano ya Kiuchumi na Mataifa makubwa.
Pili, Mauaji ya Viongozi thabiti na wenye msimamo. Hii hufanyika pale ambapo inatokea kiongozi kuwa na ushawishi mkubwa na hata kushindwa kupandikiza upinzani.
Hii ilitokea kwa Bw. Patrice Lumumba Mwaka 1961 kule Katanga na kusababisha Taifa hilo kutokuweza kutawalika mpaka sasa, vilevile iliweza kufanyika Ghana mwaka 1966 pale alipouawa Mzee wetu Kwame Nkurumah. Lakini pia Mataifa haya makubwa hutumia njia ya kuteka ama kuua wanasiasa maarufu, waandishi wa habari, viongozi wa dini na hata wanafunzi ili kuonesha kuwa utawala uliopo madarakani umeshindwa kulinda raia wake ama pia kuonesha hakuna utawala wa Demokrasia.
Njia ya Tatu ni kudumaza uchumi wa Taifa yaani kuweka Vikwazo katika maeneo muhimu ya kiuchumi. Njia hii hutumika sana na Mataifa ya Mahharibi ili kushinikiza kuangusha utawala ama utawala uliopo ukubaliane na mashariti ya kinyonyaji. Inaweza kuwa vikwazo vya kiuchumi katika Usafirishaji, uuzaji bidhaa nje kama nchi inapiga hatua za viwanda, mfano Taifa la la Chile mwaka 1973 ilifanyika hivo na kufanikiwa kuangusha utawala kwa maisha kuwa magumu na kuwapa nafasi Wapinzani kuipindua Serikali, Kinachoendelea kufanyika pale Korea ya Kaskazini ni moja ya mifano dhahiri.
Lakini pia mbali na kilichofanyika Chile na kinachoendelea kufanyika Korea ya kaskazini pia inaweza kufanyika taratibu ikiwa ni pamoja na kuzuia mali za nchi husika kwa kisingizio cha madeni wakati Taifa linaloongoza kwa kudaiwa Duniani ni Marekani ila haijawahi tokea akazuiliwa kuchukuwa mali ama bidhaa zake kutoka nchi fulani kwa sababu ya madeni.
Mbinu ya Nne, hii ni kutumia Vyombo vya habari na dini. ( MeDiaProPaGanDa ) hufanyika kwa kununua Makampuni ya Magazeti, Vituo vya Televisheni na Radio na wakati mwingine kirahisi kabisa huwanunua waandishi wa Habari na kuwawekea mifumo ya mishahara isiyo rasmi kwa kazi wanayoifanya ya kubadili ufikiri wa Wananchi kwa kuandika wakitakacho Wamagharibi.
Dini kwa kiasi kikubwa pia hutumika kwa kuwashawishi baadhi ya viongozi wa dini wenye ushawishi kuhubiri chuki dhidi ya utawala uliopo madarakani, yote hii huwa ni mbinu mahususi ya kubadili ufikiri wa wananchi maana viongozi wengi wa dini kwa asili huaminiwa na wakisemacho waumini huamini kumbe baadhi yao huwa ni mpango na mkakati wa kuingusha Serikali.
Mbinu hii kutumia dini na vyombo vya habari kwa sasa inashika hatamu kwa kiasi kikubwa ikiwa na lengo la kubadili mtazamo wa wananchi wa maeneo lengwa kwa kutumia muda mwingi kueleza mabaya pekee yasiyo halisi ya nchi za Afrika hususani Tanzania kwa sasa.
Mfano Vituo vingi vya Televisheni vya kimataifa kwa sasa wamepewa jukumu la kuzishambuliwa Nchi za Afrika zote zenye kuchukua jitihada ya kujikomboa kiuchumi ikiwepo Tanzania kwa kueleza mabaya kwa wingi pasipo uhalisia ili Wananchi husika wapoteze imani na uongozi.
Mbali na vituo vya kimataifa pia kuna baadhi ya vituo vya ndani na waandishi binafsi hulipwa pesa na kazi yao kubwa ni kukosoa kwenye kila jambo ili kubadili mtazamo wa wananchi dhidi ya Serikali yao. Mbali na Vyombo vya habari lakini pia kuna watu hudhaminiwa kufungua kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii mfano Twitter, Facebook na Instagram kwa ajili ya kusambaza taarifa za chuki na uongo kwa wananchi dhidi ya Serikali yao.
Na hili hufanyika kwa kuwa wameshatambua nguvu kubwa kwa sasa ipo katika Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Njia tano ni Kutengeneza Vurugu, maandamano na migomo. Hili hufanyika kwa ustadi mkubwa na zaidi hufanyika kwa kuwapumbaza wananchi wakaingia katika maandamano wakiwa hawajui kiundani hasa wanahitaji nini ama madai yao ni yapi dhidi ya Serikali iliyopo madarakani. Njia hii isipodhibitiwa huangusha serikali kwa maana ikatokea waandamaji wakawa wengi zaidi katika mji mmoja wanaweza kuwashinda polisi na wakaanza kufanya uhalifu, kuchoma maduka, majumba makubwa na kuchoma matairi ya gari barabarani huku wakiimba nyimbo za hamasa hatimaye Nchi inaingia katika Vurugu na hatimaye kung'oa utawala wa Haki.
Mbinu hii imewahi fanyika katika nchi kadhaa ikafanikiwa na kwa nchi thabiti ilishindwa na kwa sasa imebaki kumbukumbu kwa vizazi na vizazi.
Hii imewahi fanyika mataifa ya Misri, Libya, Iraq na ilifanimiwa miaka ya 2000 na 2010 na kwa sasa kinachoendelea kufanyika Syria ni muendelezo wa mbinu hizi chafu za Wamagharibi. Miaka ya 1970 walitaka wajaribu katika Taifa thabiti la Uchina ila Mao alisimama imara na Vijana maelfu walipoteza maisha kwa kusagwa na vifaru na sasa ni kumbukumbu njema inamulika na kuangaza kwa Taifa hilo kubwa lenye mafanikio thabiti ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Rai yangu kwa Watanzania wote wazalendo wa Taifa hili, Nchi haijengwi kwa mkate na asali ila hujengwa kwa kukubali kujikana, kukataa Unyonyaji, kuchagua Utanzania kuwa kipaumbele na kuamini kuwa kila mmoja ni mdogo kuliko Tanzania na zaidi kutambua kuwa Tanzania kuna Utawala thabiti wenye lengo la kutufikisha mahala ambapo hata vizazi vyetu havitokuja kutulaumu na kutudharau.
Yeyote anayecheza na Amani ya Nchi yetu huyo ni Adui yetu namba moja. Ni heri akatangulia kutuandalia makazi ya milele kuliko kutuchafulia Tanzania.
Tanzania ni kubwa na Nzuri kuliko mimi na wewe.
Tutunze amani yetu
Tulinde Utawala wetu.
Tunatafutwa
Ni vema tushikamane.
Imeandaliwa na;
Said Said Nguya.

ATAKAYE JARIBU KUHARIBU AMANI YETU NI HERI ATANGULIE AKATUANDALIE MAKAZI YA MILELE.*
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment