Lori lapoteza Maisha ya Mkurugenzi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhandisi Ngusa Izengo anadaiwa kufariki dunia baada ya gari lake kuangukiwa na lori la mafuta usiku wa kuamkia leo Aprili 15, 2018 katika eneo la Chalinze Nyama nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari hii na kusema atatoa taarifa kamili baada ya kukamilisha.
"Nitatoa taarifa kamili zoezi hili uokaji litakapomalizika maana mpaka muda huu tumetoka eneo la tukio tumeshindwa kujua kuna watu wangapi ndani ya gari hilo lililoangukiwa. Tunaenda TAMESA kutafuta 'grinder machine' ilituweze kujua idadi kamili ya miili iliyopo ndani ya gari", amesema Kamanda Muroto.
Lori lapoteza Maisha ya Mkurugenzi Lori lapoteza Maisha ya Mkurugenzi Reviewed by KUSAGANEWS on April 15, 2018 Rating: 5

No comments: