Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mtwara linawashikilia watuhumiwa 49 waliokamatwa katika matukio matatu tofauti
ikiwemo wahamiaji haramu 23, wezi wa pikipiki 13 na uchochezi kwa njia ya
mitandao 13.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara
Lucas Mkondya amethibitisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia wahamiaji 23 kwa
kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria. Ameeleza watu hao walikuwa kijijini
Chikongola Wilaya ya Mtwara ambapo askari wa doria walipewa taarifa na raia
wema na kufika eneo hilo.
Kamanda ameeleza kuwa mtandao wa
wezi wa pikipiki ulikuwa na kambi katika kijiji cha Chikongo wilayani
Tandahimba ambapo walikuwa wakiiba pikipiki na kwenda kuziuza kwa tajari mmoja
ambaye huzisafirisha kuziuza nchini Msumbiji.
Katika tukio lingine Jeshi la Polisi
Mtwara linawashikilia wanafunzi 9 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara na
Daktari wa Hospitali ya Mission Nanyamba halmashauri ya mji wa Nanyamba kwa
kosa la kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo ‘Watsapp’ na Telegram’ kuhamasisha
maandamano.
Watu 49 washikiliwa na Polisi Mtwara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment