Klabu ya soka ya Yanga
imekubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya Township Rollers ya Botswana kwenye
mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika jioni hii, uwanja wa taifa
jijini Dar es salaam.
Township Rollers ndio walikuwa wa
kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 11 kipindi cha kwanza lililofungwa na
Lemponye Tshireletso kabla ya Yanga kusawazisha dakika ya 30 kupitia kwa
Obrey Chirwa hivyo hadi mapumziko timu zilitoshana nguvu.
Kipindi cha pili Yanga ilianza
kushambulia kwa kasi huku Township wakionekana kujilinda kabla ya kutumia
shambulizi la kushitukiza na kuandika bao la pili dakika ya 83 kupitia kwa
Motsholetsi Sikele na kupunguza matumaini ya Yanga kuwania kitita cha bilioni
1.1 ambacho hutolewa na CAF kwa timu inayotinga hatua ya makundi.
Baada ya mchezo wa leo timu hizo
zitarudiana tena Machi 17 ambapo Yanga itasafiri hadi jijini Gaborone Botswana
kwaajili ya mchezo huo huku ikiwa na deni la kushinda mabao 2-0 au zaidi ili
kujihakikishia inatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
YANGA YAPEWA KIPIGO CHA GOLI 2 NA TIMU YA TOWNSHIP
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment