Wilaya ya Monduli mkoani arusha inakabiliwa na changamoto ya
kukatiwa maji kutokana na shirika la umeme Tanesco kuidai ofisi ya Raisi
Tamisemi deni la Shilingi milioni 115.
Akizungumza
Mbunge wa Jimbo la Monduli Julius Kalanga amesema kuwa maji
yamekuwa ya shida katika wilaya hiyo baada ya Shirika la Umeme (TANESCO) kukata
umeme kwenye chanzo cha maji Ngaramtoni kutokana na deni hilo la Shilingi
Milion 115.
Mbunge
huyo amesema wananchi hawahusiki na malipo hayo na kinachotakiwa kifanyike ni
deni hilo kulipwa ili huduma hiyo irudishwe haraka iwezekanavyo na kuepusha
kadhia zaidi kwa wananchi ya maji.
Amesema mpaka sasa ameshawasiliana na naibu
waziri wa maji pamoja na katibu wa maji ili kumaliza tatizo hilo ambalo
linaathiri wananchi pamoja na Tasisi za Elimu pamoja na Shule.
KALANGA MBUNGE"WANANCHI WANATESEKA KWA KUKATIWA MAJI"
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment