|
Serikali imetoa onyo kwa
taasisi zisizo za Serikali kuacha kupandikiza vitanzi na kuwagawia kondomu
wanafunzi shuleni kwani wanahamasisha ngono kwa umri mdogo.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 6
na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery Tesha wakati wa maonyesho ya siku mbili
ya wanawake katika viwanja vya Ghandh All.
Tesha amesema Serikali imebaini
baadhi ya mashirika na taasisi zisizo za Serikali zinazunguka na kutoa huduma
hizo shuleni
“Wanafunzi hawa tuwalee katika
maadili mema yanayostahili badala ya kuwapatia kondomu na vitu vingine
vinavyohamasisha kufanya ngono, jambo hili halikubaliki hata kidogo,” amesema
Tesha.
Mwananfunzi anayetarajia kujiunga
kidato cha tano Sada Jabiri ameiomba Serikali kuifuta sheria ya mwaka 1971
ambayo inamruhusu mtoto kuolewa akiwa na miaka kuanzia 15
“Ili kumjengea mtoto haki ya
kujitambua na kutoa uamuzi sahihi ni vyema sheria ingesema hata ianzie miaka
21 ambapo mtoto anakuwa ana ufahamu mkubwa,” amesema Sada.
Mwenyekiti wa baraza la watoto
Mkoa wa Mwanza, Neema Theonest alisema katika hali hii ya kuelekea uchumi wa
viwanda ifikapo 2025 ni vyema kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji
wanawake vijijini
Neema amewataka wanawake waache
kubweteka badala yake wajitume kufanya kazi ili kupandisha uchumi kuanzia
ngazi ya familia na kutokomeza umasikini
Akisoma risala kwa niaba ya
wanawake wa Nyamagana, Grace Saiti aliiomba Serikali iendelee kutoa fursa
nyingi za ajira kwa wanawake na kuwapatia nyadhifa mbalimbali kwani wanawake
wana uwezo wa kuongoza na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo
kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Pia amesema elimu ya masuala
ya uzalishaji na uanzishaji wa viwanda ifanyike zaidi kwenye maeneo yote ili
mwanamke hata wa kijijini afikiwe na aweze kujiendeleza.
|
Mkuu wa wilaya apiga marufuku kondomu shuleni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment