Maabara Isiyosajiliwa yafungiwa kutokana na kutoa Huduma ya afya Kinyume na utaratibu

Wananchi wa jiji la Arusha wameshauriwa kuwa makini na watu wajanja wanaotoa huduma za afya bila kufuata masharti ikiwemo baadhi ya maduka ya dawa za binadamu ,maabara binafsi na vituo vya kutolea huduma
ambavyo havifuati miongozo ya afya.

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa Jiji la Arusha Dokta Simon Chacha
wakati akifanya oparesheni ya kukagua maabara na maduka ambayo yanatoa
huduma za afya kinyume na utaratibu ambapo amefungia maabara ya ELGIBO
HEALTH iliyopo kata ya Moshono ambayo ilikuwa imefanywa kama zahanati na haijasajiliwa na
mamlaka husika.

Dokta Chacha amesema kwenye ukaguzi huo amesema maabara hiyo inaendeshwa na mtu ajulikanaye kwa jina la Jaled Onesmo Macha ambaye
ni tabibu ambapo anawaandikia wagonjwa vipimo na kuwaelekeza kwenda kununua dawa kwa bei ghali kwenye duka lake la jirani na maabara
liitwalo J D MEDICS.

Kufuatia hayo Dokta Chacha amelifungia pia duka hilo kwa kukosa vigezo
na hakuna mtaalamu ambaye anajua masuala ya dawa na halijasajiliwa
pamoja na kuuza dawa zisizoruhusiwa.
Maabara Isiyosajiliwa yafungiwa kutokana na kutoa Huduma ya afya Kinyume na utaratibu Maabara Isiyosajiliwa yafungiwa kutokana na kutoa Huduma ya afya Kinyume na utaratibu Reviewed by KUSAGANEWS on March 06, 2018 Rating: 5

No comments: