Taarifa zilizoenea
mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP),
Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana
saa sita usiku.
Marafiki za Nondo
wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na
baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea
chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp.
Taarifa kutoka kwa
mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi
wake.
Viongozi wa TSNP
wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na
kutoa taarifa za kupotea kwake.
February 18, 2018,
Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya
Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri
Mwigulu Nchemba ajiuzulu.
Akizungumza na
wanahabari jana March 6 2018, Nondo aliwataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa
wizara na serikali na kuwataka wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea
wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.
“TAHLISO ambayo kila
chuo kikuu nchini kinatoa ada isiyopungua shillingi laki tano kwa mwaka ili
TAHLISO iweze kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, imeacha
kutimiza wajibu wake wa msingi na badala yake imegeuka kuwa taasisi yenye
kusema kwa niaba ya serikali pamoja na kushambulia taasisi ambazo zinatetea
maslahi ya wanafunzi nchini ikiwemo TSNP.
“Akwiline alikuwa ni
mwanafunzi pia, TSNP ni mtandao wa kutetea wanafunzi, tunayo hayo mamlaka
kusemea, kukemea, kushauri na hata kutoa mapendekezo yetu juu ya tukio lolote
linaloashiria upotevu wa haki kwa wanafunzi. TAHLISO wanatoa wapi
ujasiri, mamlaka ya kutuzuia TSNP tusitimize wajibu wetu?” alisema Nondo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Abdul Nondo Apotea Gafla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment