![]() |
![]() |
| Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akimtwisha Mwananchi ndoo ya maji leo , wanao shuhudia tukio hilo ni Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam. |
NA CHRISTINA MWAGALA
WANANCHI wa Kata ya Pugu, Mtaa wa Mustafa, wamempongeza Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kwa kuwapelekea maji safi na salama huku wakibainishiwa kuwa ameweka historia ya kutatua changamoto hiyo.
Kata hiyo ambayo inadaiwa kuongoza kwa
changamoto ya maji kwa kipindi kirefu, imejenga historia leo kupitia kwa Meya
Mwita ambaye amepeleka maji na hivyo wananchi hao kuondokana na adha hiyo
iliyodumu kwa kipindi kirefu.
Meya Mwita ameahidi pia kuongeza huduma
hiyo kwenye maeneo ambayo yanachangamoto ya maji.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mtaa
huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mustafa Bahati Lusizi alimshukuru Meya
Mwita kwa juhudi alizozionyesha hadi kufanikisha kuwapatia huduma
hiyo kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu.
Amesema tangu kuingia kwa uongozi wake
umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba waliomba kwa kipindi kifupi kupatiwa
maji huduma hiyo na hivyo wameweza kutekelezewa kwa wakati walioahidiwa.
Alifafanua kuwa kwa sasa wananchi wa eneo
hilo wanapata maji safi na salama, nakuomba kufikishiwa kwa huduma hiyo maeneo
mengine yenye changamoto hizo.
“ Kwaniaba ya wananchi wa mtaa huu,
tunakupongeza Meya umefanya kazi kubwa, eneo hili linachangamoto ya maji,
lakini kwa sasa itakuwa historia ,kwenye huu utawala wako tutakukumbuka kwa
kutuondolea kero hii” amesema Lusizi.
Awali Meya Mwita akizungumza na madiwani,
wananchi walioshuhudia mradi huo wa maji, amesema kuwa juhudi zilizofanyika
katika eneo hilo, zitatumika kwenye maeneo mengine ili kila mwananchi wa kata
hiyo aweze kunufaina na kuondokana na kero hiyo.
Meya Mwita amewaelekeza viongozi hao
akiwemo Diwani wa Kata hiyo Boniventure Mphuru hadi kufikia Aprili Mwaka huu,
wananchi hao wapate huduma hiyo ya maji kwa bei ya shilingi 50 kwa kila ndoo
badala ya sh.100 ambayo wanauziwa kwa sasa.
“ Nia yangu katika nafasi niliyonayo ni
kuhakikisha kwamba kero mbalimbali zinazo wakabili wananchi ninazitatua, Kata
ya Pugu inachangamoto sana ya Maji, lakini sasa ninawaambia itakuwa historia
kwenye uongozi wangu” amesema Meya Mwita.
Wakati huo huo, Meya Mwita ameridhishwa na
ujenzi wa ukuta wa Dampo la Pugu Kinyamwezi unaoendelea hivi sasa ambapo
wakandarasi wanaojenga ukuta huo wamemtoa wasiwasi wa kieleza kuwa ujenzi huo
hautakuwa na madhara kwa wananchi waliopo karibu na eneo hilo.
Aidha mbali na ujenzi huo wa ukuta, lakini
pia ameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege
yenye urefu wa kilomita 0.7 kuingia kwenye Dampo hilo ambapo
utawezesha barabara hiyo kupitika kwa kipindi chote cha mwaka bila tatizo lolote.
Wananchi wa Pugu wa mpongeza Meya Mwita kwa kuwapatia maji safi na salama.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:






No comments:
Post a Comment