Na
Ferdinand Shayo,Arusha.
Wilaya
ya Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa
maziwa mkoani Arusha,maziwa ambayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya
Jiji la Arusha na nje ya jiji hilo.
Licha
ya uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo hivyo kupelekea maziwa
wanayoyazalisha kuharibika baada ya kukaa muda bila kununuliwa.
Kufuatia
Changamoto hiyo Moja kati Daktari wa Mifugo Dokta Deo
aliona changamoto hiyo kama fursa ya uwekezaji kwani malighafi ya maziwa
inapatikana kwa wingi ,kwa kuwa wafugaji walikua wakiyamwaga maziwa yao
yaliyokua yakiharibika kwa kukosa soko la uhakika na hawakua na
namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila
kuharibika.
Dokta
Deo aliacha kazi ya kuajiriwa mwaka 2001 na kuamua kufuga ng`ombe
1 baadae wawili ambao walikua wakitoa lita 40
kila siku huku yeye na familia yake wakitumia lita 1 hivyo maziwa mengine
kuharibika baada ya kukaa kwa muda.
Suala
hili lilimfikirisha sana Dokta Deo ambaye alimtafuta mtaalamu kutoka nchini
Kenya atakayemfundisha jinsi ya kuongeza thamani maziwa yake
,kuyafungasha na kuyauza .Mtaalamu huyo alimfundisha ndipo akaianza kazi ya
kuongeza thamani maziwa hayo nyumbani kwake.
Baada
ya muda majirani zake wafugaji walianza kuvutiwa na jinsi anavyoongeza thamani
maziwa yake na walimletea maziwa ili ayaongeze thamani ndipo alipoanza kununua
maziwa na kuongeza thamani takribani lita 100,150 mpaka 200 kwa siku.
Baada
ya hapo akafungua kiwanda kidogo ambacho kilikua na uwezo wa kusindika lita
200 kwa siku huku wafugaji wakileta maziwa mengi
zaidi ndipo alipoongeza uzalishaji na kwa sasa anazalisha lita 2000
kwa siku.
Kutokana
na ongezeko hilo lauzalishaji kwa sasa Dokta Deo pamoja na Wakurugenzi wenzake
wa kiwanda hicho cha The Grande Demam wameongeza wigo na kununua maziwa zaidi
kwa wafugaji ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga
maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.
Kiwanda
hicho kinanunua maziwa bora kutoka kwa wafugaji na kuyaongezea thamani ikiwa ni
pamoja na kuyafungasha vyema.
“Maziwa
ambayo hayajaongezwa thamani hukaa kwa muda wa masaa 13 lakini maziwa
yaliyoongezwa thamani yanaweza kukaa hadi mwezi mmoja jambo ambalo linaleta
unafuu hasa kwa kipindi kifupi kabla hayajafika sokoni” Alisema
Dokta Deo
Dokta
Deo anaeleza kuwa maziwa yaliyosindwa ni maziwa mazuri kwa afya ya binadamu
yamekua yameondolewa bacteria hatarishi na kuongezewa bacteria rafiki kwa afya.
Mtu
anayetumia Maziwa ambayo hayajasindikwa anakua yuko hatarini kupata magonjwa
mbalimbali ikiwemo Tb,Typhoid na Brusela.
Pia
maziwa yaliyosindikwa kiwandani yanasaidia kupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu.
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho Dokta Deo amesema kuwa maziwa ni bidhaa yenye faida kubwa sana
katika mwili wa binadamu ikiwemo virutubisho aina ya Protini,Madini,Fat pamoja
na wanga.
Dokta
Deo anashauri unywaji wa maziwa uhamasishwe kwa wingi katika jamii ili kuwa na
jamii yenye afya bora inayoweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji.
Anaeleza
kutokana na ubora wa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho wateja wamekua
wakiyafurahia hivyo wanafirikiria kuongeza uzalishaji na kuboresha zaidi ili
kuwafikia wateja wengi zaidi.
“Tuna
mpango wa kuzalisha mpaka lita laki moja kwa siku ,uzalishaji huu utaleta tija
kwa kiwanda pamoja wafugaji ambao tumekua tukinunua maziwa kwao tutanunua
maziwa mengi zaidi hivyo kukuza kipato cha wafugaji waweze kunufaika na
shughuli zao za ufugaji” Alisema Dokta Deo
Ni
vyema Watanzania wakajifunza kunywa maziwa haya bora yanayozalishwa
nchini badala ya kunywa maziwa kutoka nje kwani kwa kufanya hivyo utakua
unainua uchumi wa nje.
Biashara
hiyo ya maziwa imesaidia vijana wengi waliojiriwa na kiwanda hicho
katika sekta ya uzalishaji na usambazaji jambo ambalo linaonyesha mnyororo wa
wanufaika wa kiwanda hicho unavyoongezeka.
Kwa
sasa bidhaa za maziwa,Yogat na Siagi za The Grande Demam imefika
katika mikoa ya Dar es Salaam ,Manyara ,Tanga na Morogoro.
Mshauri
wa Masuala ya Biashara katika Kiwanda Peter Ojukwu hicho
amesema kuwa kiwanda hicho kinaweza kuwanufaisha watu zaidi ya 4500 kutokana na
mzunguko wa uzalishaji mpaka kumfikia mlaji.
Anaeleza
kuwa licha ya kiwanda hicho kujikita na uzalishaji wa maziwa bado kinatoa
huduma za ushauri wa ufugaji bora,matibabu ya mifugo pamoja na madawa ili
waweze kufanya ufugaji wenye tija.
Pia
anashauri serikali na taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Wawekezaji
wanaowekeza kwenye viwanda ikiwamo kiwanda cha maziwa kwani kinagusa maisha ya
watu wengi moja kwa moja.
“Kama
unavyojua katika maziwa hakuna kinachosalia unatoa
maziwa,siagi,yogati,samli,mtin di hivyo hakuna kinachotupwa kila
kitu kina thamani kubwa” alisema Mshauri huyo
Nassari
na ni moja kati ya Wafugaji ambao maziwa yao yananunuliwa na kiwanda hicho
wamesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho wamekua wakipata soko la
uhakika la maziwa yao hivyo kuondokana na tatizo la maziwa
kuharibika kwa kukosa soko.
Anaeleza
kuwa uwepo wa kiwanda hicho umewasaidia wafugaji wengi ambao walikua hawana pa
kuyapeleka maziwa yao lakini kwa sasa wanafika katika kiwanda hicho na
kuyapeleka maziwa yao.
0765938008
THE GRANDE DEMAM KIWANDA CHA MAZIWA KINACHOWANUFAISHA KIUCHUMI WAFUGAJI 2000
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment