Mbunge wa Arusha Mjini
(CHADEMA), Godbless Lema amesema ipo haja ya yeye kuzungumza katika kikao
kijacho cha Bunge juu ya hoja binafsi iliyowasilishwa na Mbunge mwenzake
Hussein Bashe siku ya Jana (Machi 5, 2018).
Lema ametoa kauli hiyo kupitia
ukurasa wake maalumu baada ya kupita siku moja tokea Mbunge Bashe kupelekea
barua hiyo kwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka iundwe
kamati Teule ya kuchunguza baadhi ya mambo yanayoendelea katika ardhi ya
Tanzania.
"Nina fikiri ninapaswa kusema
kidogo juu ya hoja binafsi ya Mhe. Husein Bashe katika mkutano wa Bunge
unaokuja. Hivi ni kweli tunahitaji Kamati teule kuhusu utekaji na kufifia kwa
demokrasia nchini. Ni maamuzi ya CCM katika mikutano yao ya ndani ya Bunge na
nje ya Bunge kuhusu hali ya demokrasia na siasa nchini, ujenzi wa vyama vya
siasa na mikutano imepigwa marufuku", amesema Lema.
Pamoja na hayo, Lema ameendelea kwa
kusema "wakati mambo haya yanaendelea kutokea Bunge limekataa
hata kulipa matibabu ya Mh Lissu. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CCM akiwemo
Husein Bashe aliyewahi kwenda kumjulia hali Mh Lissu Hospital, najiuliza ni kwa
nini ?. Mambo haya yako wazi hayahitaji PHD kujua msimamo wa Wabunge wa CCM
kuhusu haki, ukweli na nuru ya mabadiliko".
Aidha, Lema amedai endapo Wabunge
kutoka chama tawala wakibadili mtazamo wao kuhusu nchi basi hata Bunge litakua
imara ambapo ndio msingi wa serikali bora unaotokana na wabunge majasiri.
"Bashe unafikiri Kamati Teule
inaweza kuwa na maana kwenye Bunge hili ? hotuba za wapinzani Bungeni
zimeendelea kuwa 'sensored' ndani ya Bunge na haya ni maoni mbadala ya ushauri
kwa serikali lakini siku zote mmekaa kimya. Tunahitaji umoja wenu kwa masilahi
ya haki ndani ya Bunge kwenye mambo yote yanayorudisha heshima ya Wabunge,
wingi wenu umekuwa hasara kwa nchi badala ya faraja", amesisitiza Lema.
Lema ameendelea kusisitiza
"Tunapoona maigizo yanayotaka
kupotosha haki yanazingatiwa hapa ndipo tunapatwa hasira na kuondoa nidhamu
katika mahusiano yasiyo na tija na nchi, hata hivyo andiko hili sio ugomvi
lakini pia limejengwa hasira na hali zetu kisiasa tunayopitia, sisi Wabunge wa
upinzani karibu wote tuna kesi sehemu mbali mbali nchini mmoja wetu sasa ni
mfungwa (Sugu)".
Kwa upande mwingine, Mbunge Godbless
Lema amesema wanapitia katika maumivu makali katika siasa wanazozifanya hivyo
hawaitaji kuona sinema tena zikiendelea kutoka kwa miongoni mwa wabunge wenzao.
"Tunapitia katika maumivu makali katika siasa" Mbunge Lema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment