Baada ya klabu ya Manchester
United kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 jana usiku dhidi ya
Crystal Palace, mechi hiyo imeacha rekodi mbalimbali katika ligi kuu ya
England.
Moja ya rekodi ni klabu ya
Manchester United kutokea nyuma kwa mabao 2-0, na kushinda mchezo wa Ligi
Kuu kwa mara ya kwanza tangu ifanye hivyo Desemba 2013 ugenini dhidi ya Crystal
Palace.
Kwa upande wa Crystal Palace jana
ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza kupoteza baada ya kuwa wanaongoza kwa mabao
2-0 au zaidi. Pia Crystal Palace hawajashinda mechi 20 sasa dhidi ya United
ikiwa ni idadi kubwa ya mechi kuliko timu zote walizokutana nazo.
Rekodi nyingine ni bao la kwanza la
Nemanje Matic kwa tangu ajiunge na United huku likiwa ni bao la ushindi la
dakika ya 90 kwa United tangu alipofunga bao la ushindi Marcus Rashford
dakika ya 90 dhidi ya Hull City mwaka 2016.
Man United na Crystal Palace zaacha rekodi hizi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment