Mabingwa wa soka nchini
klabu ya Yanga itaanza kibarua cha kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano
ya Ligi ya Mabingwa Africa, hatua ambayo itawawezesha kujikusanyia kiasi cha
shilingi bilioni 1.1,kama wataitoa Township Rollers ya Botswana.
Yanga leo jioni watakuwa wenyeji wa
Township Rollers kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni mechi ya
kwanza Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, kuanzia Saa
10:00 jioni.
Kwa mujibu wa utaratibu wa
Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu zinazofuzu hatua ya makundi
zinajihakikishia kupata bilioni 1.1 na zinakwenda kuwania fedha zaidi kulingana
na matokeo yake kuanzia hatua hiyo.
Kwa timu zitakazofuzu hatua ya Robo
Fainali zinajihakikishia kupata shilingi bilioni 1.3 huku zile zitakazofika
nusu fainali zinapata shilingi bilioni 1.7 huku bingwa akipata zaidi ya bilioni
2.5 na bingwa akijikusanyia bilioni 3.
Yanga imewahi kufika hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa mara moja tu, mwaka 1998 katika mfumo wa zamani wa
kuanzia hatua ya Robo Fainali, wakati kwenye Kombe la Shirikisho pia ilifika
hatua ya makundi mwaka 2016.
Yanga kusaka bilioni 1 leo kama wataitoa Township Rollers
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment