Upelelezi
wa kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Ujangili, Wayne Lotter inayowakabili
watu 8 akiwemo Ofisa wa Benki ya NBC Makao Makuu katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi
Mkuu, Wilbard
Mashauri na Wakili wa serikali, Adolph Mkini ambapo
ameeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, anaomba kesi ipangiwe
tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri
ameahirisha kesi hiyo hadi March
21,2018 kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.
Awali katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa
watatu 3 ambapo sasa wapo 8 baada ya kuunganishwa katika kesi hiyo.
Katika kesi hiyo washtakiwa ni Nduimana Jonas (40) ‘Mchungaji’
ambaye ni raia wa Burundi, Godfrey Peter (42) mfanyabiashara, Innocent Pius
(23) mfanyabiashara, Chambie Juma (32) mfanyabiashara na Robert Harride (31)
Ofisa wa Benki ya NBC.
Pia mfanyabiashara Rahma Almas ‘baby'( 37 ),
Mohammed Maganga (61) ambaye ni mchimba makaburi
na Khalid Almas
(33).
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili
ikiwemo kutenda kosa la kula njama ya kufanya mauaji ya Mwanaharakati wa
kupinga Ujangili, Wayne Lotter katika tarehe tofauti kati ya July 1,2017 na August 16,2017.
Katika kosa la pili washtakiwa hao
wanadaiwa kuwa, katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie
Kinondoni DSM August 16, 2017 walimuua Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza
wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter (52).
Watuhumiwa 8 wa Kesi ya Ujangili bado haijakamilika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment