Wizara ya Afya yatia saini mkataba wa ushirikiano

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim pamoja na Balozi wa Taifa la Palestina nchini Tanzania Hazem Shabat wametia saini ya mkataba wa ushirikiano kwenye sekta ya afya.

Kupitia mkataba huo Taifa la Palestina pia litasaidia katika kuleta madaktari kwa ajili ya kutibu magonjwa yakiwamo ya uti wa mgongo ambapo madaktari wao na wa Tanzania watafanya kazi pamoja ya kutoa huduma za afya.


Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri Mwalim amesema kuwa wanatambua kuna changamoto katika kutibu baadhi ya magonjwa nchini, hivyo madaktari bingwa wa Palestina na madaktari bingwa waliopo nchini watatumia fursa ya mkataba huo wa ushirikiano katika kutoa huduma za tiba kwa Watanzania.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano,chini ya Rais, Dk.John Magufuli imekuwa na jitihada  mbalimbali za kuboresha sekta ya afya lakini mkataba uliotiwa saini leo unatoa fursa ya kuimairisha pia utoaji wa chanjo na dawa.

Amesema mkataba huo umejikita kwenye maeneo mbalimbali na baadhi ni kusaidia katika kutoa huduma za afya, kusaidia upatikanaji wa dawa, kuimarisha eneo la Tehama ili kuboresha huduma hasa kwa kuzingatia teknolojia ya habari na mawasiliano itasaidia kuimarisha mfumo wa kutunza kumbukumbu za sekta ya afya.


Wizara ya Afya yatia saini mkataba wa ushirikiano Wizara ya Afya yatia saini mkataba wa ushirikiano Reviewed by KUSAGANEWS on March 05, 2018 Rating: 5

No comments: