Chma cha CHADEMA kimesema kufuatia kauli ya Cyprian Musiba kudai CHADEMA inashirikiana na nchi za Marekani na Ujerumani kuhatarisha Usalama wa Taifa, hivyo kimeziandikia barua nchi hizo kutoa maelezo na kuitaka serikali iseme Musiba ametumwa na nani.
Akizungumza na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- CHADEMA bwana John Mrema amethibitisha na hilo na kusema wameamua kuchukua hatua hiyo kuzitaka nchi hizo zitoe kauli dhidi ya kauli hiyo kwani ni kauli ambazo hazitakiwi kufumbiwa macho
"Ni kweli tuliwaandikia rasmi ubalozi wa Marekani na Ubalozi wa Ujerumani kwa sababu ndugu Musiba alihusisha balozi hizo kwamba zimekula njama na CHADEMA ama kufundisha watu au mashirika yao ya ujasusi kwa ajili ya kuleta maafa kwenye nchi sasa tumezitaka balozi hizo zieleze kwa sababu tukisema sisi tutaonekana tunajitetea na ziiulize Serikali ya Tanzania Musiba ametumwa na nani"
Aidha Mrema aliendelea kueleza kuwa jambo ambalo amefanya Musiba si jema lakini anashangaaa kuona vyombo vya usalama mpaka sasa hakuna hatua yoyote zinachukua juu ya mtu huyo.
"Tumeandika barua hizo toka wiki iliyopita na zimepokelewa pamoja na CD yenye matamshi ya Musiba, hili ni jambo la hatari katika nchi inavyotokea raia anaweza kuchafua tu nchi nyingine akaachwa na vyombo vya dola havichukui hatua ni jambo ambalo si jema kwa diplomasia yetu na mahusiano yetu mataifa makubwa kama Marekani na Ujerumani mtu anaibuka anasema zimefundisha vijana 500 wa CHADEMA hao vijana walipita wapi? kwa sababu Airport ya Dar es Salaam sidhani hata kama uhamiaji wamewahi kutoa passport 500 wa watu wa CHADEMA kwa hiyo huu ujinga ujinga usiposhughulikiwa yatakuwa ndiyo utamaduni wetu jambo ambalo ni la hatari kwa nchi" alisema Mrema

Chadema waandika Barua kufuatia kauli ya Musiba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment