Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi leo jijini Dar es Salaam asubuhi huku Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akishindwa kuripoti kutokana na ugonjwa unaomsumbua.
Wakili wa Chadema Alex Massaba, amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hawezi kuripoti Polisi kwa sababu anaumwa, hata hivyo hakuweka wazi ugonjwa unaomsumbua Mwenyekiti huyo.
Viongozi hao wamewasili kituoni hapo kutokana na wito waliopewa wa kuripoti kituoni hapo wiki iliyopita na kutakiwa kurudi leo ambapo waliongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt.Vicent Mashinji.
Wengine walioripoti kituoni hapo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Viongozi hao wamewasili kituoni hapo saa 1:25 asubuhi wakisindikizwa na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya.

Viongozi wa Chadema wafika Polisi bila Mbowe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 05, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment