Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amekagua mradi wa usambazaji wa maji kwenye vijiji vinavyopitiwa na
mradi wa maji Mbwinji na ameridhishwa na unavyoendelea.
Waziri Mkuu alifanya ukaguzi huo
katika kioksi cha kuchotea maji kilichopo kwenye kijiji cha Mbecha wilayani
Ruangwa na kusema mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa
Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) unatarajiwa kukamilika Machi 31, 2018.
"Huduma ya upatikanaji wa maji
safi na salama kwa wananchi ni miongoni mwa vipaumbele vya serikali ya awamu ya
tano, hivyo vijiji vyote vitapata maji. Serikali ya awamu ya tano ina mikakati
mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika
maeneo yote yenye tatizo hilo nchini", amesema Majaliwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema vijiji
ambavyo vimenufaika na mradi huo wilayani Ruangwa ni sita ambavyo ni Chiyapi,
Nandanga, Ipingo, Lucheregwa, Litama na Mbecha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji
wa MANAWASA Mhandisi David Mwamsojo amesema mradi huo utagharimu sh. milioni
870.738 hadi kukamilika na kuhusisha vijiji 12 vilivyo kwenye umbali wa
kilomita tano kutoka kwenye bomba kuu pamoja na ujenzi wa vioksi 18 vya
kuchotea maji.
Waziri Mkuu afanya ukaguzi wa maji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 02, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment