Mganga mkuu wa jiji la Arusha
Simon Chacha amelifungia duka la Divine Medics and Cosmets kwa
kuchanganya biashara ambapo anauza Dawa za binadamu na viatu vya Yeboyebo
jambo ambalo liko kinyume na sheria za afya.
|
Dokta Chacha amesema
kuwa hakuna utaratibu unaoruhusu mfanyabiashara kuchanganya Dawa ambazo
wanatumia binadamu kwa afya na humo humo kunauzwa viatu pamoja na Vyombo vya
matumizi ya nyumbani.
Amesema Sheria za afya
zinaelekeza pale mtu unapopatiwa kibali cha kuuza dawa lakini wengi wao hukiuka
maelekezo yaliopo wanafanya wanavyojua wao.
"Anachokifanya siyo
sawa na kuna sababu zinazofanya kufungia hii biashara kwanza Anachanganya
biashara viatu na vyombo pili anatibu tatu anauza Dawa zisizoruhusiwa kuuzwa
na mamlaka husika na nne anapima malaria duka chafu na hafuati
miongozo"Alisema Dokta Chacha
Hata hivyo amesema kuwa
hakuna kitu ambacho kinatakiwa kuangaliwa kwa umakini kama vitu vinavyotumika
kwenye mwili wa binadamu na kila atakayeenda kinyume na sheria walizokubaliana
na mamlaka husika.
"Tunachotaka
taratibu zifuatwe kwa hawa wenye maduka ya dawa za binadamu kwasababu
wanapokosea kumpa mtu dawa bila kibali maalum akipata matatizo sisi wasimamizi
tuna yakujibu sasa hatutaki yatokee hayo yote tunachotaka maelekezo yafuatwe
tu"Aliongeza Dokta Chacha
Kwa upande wa mmliki wa
Duka Hilo lililofungiwa la Divine ameshindwa kutoa majibu sahihi kwanini anauza
vitu hivyo kinyume cha utaratibu unaowaongoza.
Mpaka sasa maduka zaidi
ya 20 katika jiji la Arusha yamefungiwa kutokana na kutokidhi vigezo pamoja na
kwenda kinyume na Miongozo ya wizara ya Afya.
|
No comments:
Post a Comment