MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASILIMIA 80 YA WANAWAKE WANAOGOPA KUKOPA KWASABABU YA KUFILISIWA MALI ZAO


 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu akiwa na akina mama wa soko la lokii kata ya bwawani akisikiliza changamoto za wanawake wafanyabiashara.



 Mwenyekiti wa UWT Yasmini Bachu akizungumza na mmoja wa akina mama wafanyabiashara

Mwenyekiti wa UWT Yasmini Bachu akiwa amekaa kwenye kibanda cha mwanamke mmoja mfanyabiashara akinywa uji aina ya Loshoro
 Mwenyekiti wa UWT Yasmini Bachu akiwa amekaa chini kusikiliza wanawake wafanyabiashara 
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu ameendelea na ziara yake ya siku ya pili katika soko la Lokii lililopo katika kata ya Bwawani halmashauri ya Arusha na kutaka wanawake kutoogopa kujiunga na vikundi vya kukopa hasa mikopo inayotolewa na halmashauri Asilimia 5.

Akizungumza baada ya kupata malalamiko kwa wanawake wafanyabiashara katika soko hilo wanaotoka kwenye kata zaidi ya kumi Bachu amesema asilimia 80 ya wanawake wanaogopa kukopa kutokana na suala la kufilisiwa kwasababu wengi wao walijiunga na vikundi vya mitaani.

“Kilicho hapa ni kwamba wengi wanaogopa kufilisiwa wengine,kutoaminiana kwasababu wengine wanalazimishiwa kuchukua mkopo kwa lazlima kama laki 5 milioni moja sasa unakuta hutaweza kurudisha msikate tamaa kwa yaliyotokea mitaani na sasa pesa zipo halmashauri lakini hakuna vikundi vipya ndiyo maana tumekuja huku sokoni halmashauri ina pesa nyingi na kwa mwaka mikopo inatoka mara 6 mnatakiwa mje mchukue ”Alisema Yasmini Bachu

Amesema kuwa wengi wao wamefilisiwa na watu kutokana na kuchua mikopo kwa watu binafsi mwisho wa siku kuuziwa nyumba ,mashamba na vyombo ndani kwasababu ya Riba kubwa wazowekewa na masharti magumu.

Hata hivyo Bachu amewapa moyo akina mama hao kutoogopa tena kwasababu serikali ya awamu ya tano kupitia Raisi Magufuli wameamua kusikia vilio vya akina mama kwasababu ndiyo wanaobeba familia wakaamua kutoa mikopo ambayo haina masharti magumu ambayo dhamana yake ni kujiunga tu kwenye vikundi vya watu 5 au kumi na kwenda kwa viongozi wa vijiji kwa ajili ya kupewa mikopo.

Awali wakitoa malalamiko yao kwa mwenyekiti akina mama a hao wamesema kuwa mpaka sasa wengi wao wamefilisiwa hivyo anapokuja mtu kuwahamasisha kukaa kwenye vikundi wanahisi ni mambo yaleyale jambo ambalo Bachu amelitolea ufafanuzi kuwa mikopo ya halmashauri ina riba nafuu kabisa .

Wameongeza kuwa kuna baadhi ya watumishi wa serikali wamekuwa matapeli kwa kuwarubuni akina mama kujiunga na vikundi na kutoa pesa baadaye kutosajiliwa ile hali wameshatoa pesa zao za kujisajili.

Mwenyekiti Yasmini anaendelea na ziara yake ya kutembelea wafanyabiashara Kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto za kina kwa mama wafanyabiashara ndogondogo kabisa masokoni na minadani ,mbogamboga na mama lishe ambao mitaji yao ni midogo na kuziwasilisha kwa serikalini halmashauri na mamlaka zingine.

Hata hivyo ni katika  kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo inaanza tarehe mosi mwezi wa 3 ambapo kilele chake ni tarehe 8 mwezi wa tatu

MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASILIMIA 80 YA WANAWAKE WANAOGOPA KUKOPA KWASABABU YA KUFILISIWA MALI ZAO MWENYEKITI UWT MKOA WA ARUSHA ASILIMIA 80 YA WANAWAKE WANAOGOPA KUKOPA KWASABABU YA KUFILISIWA MALI ZAO Reviewed by KUSAGANEWS on March 02, 2018 Rating: 5

No comments: