Arusha. Makatibu wakuu wa wizara
15 pamoja na baadhi ya watendaji wa wizara hiyo watembelea Ziwa Manyara kuona
hali halisi ya uharibifu wa ambao unatishia kukauka kwa ziwa hilo.
Mwenyekiti wa makatibu wakuu hao,
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Maimuna Tarishi amesema lengo la ziara hiyo
ya kazi ni kujionea uharibifu wa ziwa na kuishauri Serikali.
Amesema hivi karibuni mawaziri
ambao wizara zao zinahusiana na ziwa hilo walikutana na kupokea changamoto za
ziwa hilo na waliagiza makatibu wakuu kutembelea na kupata hali halisi na
baadae kuishauri Serikali.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (Tanapa), Allan Kijazi amesema ziwa Manyara lipo hatarini
kukauka kutokana na kuongezeka shughuli za kibinaadamu pembezoni mwa ziwa.
Amesema shughuli hizo pia
zimeathiri mapito na mtawanyiko wa wanyama katika eneo la ikolojia ya hifadhi
za Manyara na Tarangire.
Ziara ya makatibu wakuu inaendelea
muda huu na inashirikisha watendaji wa Serikali, ofisi ya mkuu za wakuu wa
mikoa Arusha na Manyara, ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali na maofisa
wa wizara hizo
|
MAKATIBU WAKUU 12 WATEMBELEA ZIWA MANYARA ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment