Kundi la vijana 29
wanaodaiwa kufanya uhalifu mkoani Mbeya maarufu kama wakorea weusi wamekamatwa
na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhaulifu, kupiga, kuua na
kuibia watu vifaa mbalimbali.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi, Mohammed Mpinga amewaambia
wanahabari ofisini kwake leo, Jumamosi kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea
kuhojiwa na wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi
utakapokamilika.
Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane kutokana na kujihusisha na
vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao
walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.
Kwa upande mwingine, Kamanda MPINGA ametoa
wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu
kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa
ajili ya kujipati kipato.
Jeshi la Polisi lakamata kikundi cha wauaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment