Jeshi la Polisi mkoani
Dodoma linawashikilia wahamiaji haramu wawili raia wa Rwanda pamoja na watoto
20 wa mitaani wenye umri kati ya miaka 7 hadi 15 ambao wamekuwa wakitumiwa na
wahalifu kuiba vifaa mbalimbali vya magari.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Dodoma Giles Muroto akizungumza na waandishi wa habari mjini
Dodoma , amesema katika msako uliofanywa tangu Februari 28 mwaka huu,
wamefanikisha kukamatwa kwa wahamiaji wawili na watoto hao ambao wamekuwa
wakitumia dawa za kulevya aina ya gundi.
Kamanda huyo amesema wazazi wa watoto hao wanapaswa kufika
kituoni kuwachukua watoto hao ili kuepusha kushtakiwa kwa mujibu wa sheria kwa
kushindwa kuwalea watoto wao.
Aidha amesema pia katika msako huo jeshi hilo limewakamata
wahamiaji haramu wawili februari 28, mwaka huu ambao ni raia wa Rwanda katika
'check point' ya polisi mtera wilayani Mpwapwa barabara ya kuelekea Iringa.
Jeshi la Polisi Dodoma lawashikilia wahamiaji Raia wa Rwanda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment