Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa ufuta katika mikoa inayolima zao hilo nchini kuuza kwa kutumia njia ya minada na si mashambani.
Ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Nachihungo, Narungombe na Chikwale.
Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi amesema ili wakulima waweze kupata tija ni vema wakauza ufuta wao kwa kupitia minada kama inavyofanyika katika zao la korosho
“Usikubali kumuuzia mtu yeyote ufuta wako ukiwa shambani kwa sababu bei atakayonunulia ni ndogo kulinganisha na soko, naamini ufuta wote ukiuzwa katika minada mtaona faida.”Majaliwa
Kufuatia agizo hilo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue aandae utaratibu wa maeneo ya kukusanyia ufuta na kufanyia minada.
Amesema ufuta unaolimwa nchini ni bora na unapendwa sana duniani hivyo wasiwe na wasiwasi.
Baadhi ya Mikoa inayolima ufuta kwa wingi ni Lindi, Pwani, Dodoma, Manyara, Kigoma na Singida.

Majaliwa apiga marufuku uuzwaji wa Ufuta
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment