Jumuiya ya Taasisi za
Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) imewataka wanafunzi wote wa vyuo
vikuu nchini kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na uchunguzi wa kifo cha
Akwilina Akwilin aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, mwaka huu.
Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti
wa Seneti ya TAHLISO, George Mnali wakati akizungumza na waandishi wa habari
mjini Dodoma kuhusiana na msimamo wa Jumuiya hiyo kuhusu kifo cha mwanafunzi
mwenzao huyo.
Mnali amesema kuwa wanafunzi wa vyuo
vya elimu ya juu nchini wanapaswa kuwa watulivu na wavumilivu wakati
vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi wake kuhusiana na kifo hicho kama
ambavyo wameendela kuwa watulivu.
Mbali na hilo amevitaka vikundi
mbalimbali ambavyo vimejitokeza kuwasemea wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu
kuacha mara moja tabia hiyo kwa kuwa chombo pekee cha kuwasemea wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu ni TAHLISO peke yake.
Ameongeza kuwa wamegundua
vikundi hivyo vinatumika kisiasa na vina lengo la kuharibu amani ya nchi kwa
kuwa vinawataka baadhi ya viongozi kujiuzulu na wakati hata matokeo ya uchunguzi
wa tukio hilo bado haujatoka.
Pia amewatupia lawama wanasiasa kwa
kushindwa kulinda kauli zao ambazo ndizo zilikuwa chanzo cha tukio hilo.
Wamafumzi Waonywa kuhusu kifo cha Akwilina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment