Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi amewasisitiza askari kuepuka ubambikaji
kesi kwa wananchi, rushwa na ubabaishaji pia akiwataka askari kufanya kazi kwa
utii, nidhamu na maadili kama ambavyo Jeshi la Polisi Tanzania linavyoelekeza.
Hayo yamejiri tarehe 28/02/2018
wakati Kamanda Msangi alipokutana na askari wa Wilaya ya Sengerema katika
ukaguzi anaoendelea kuufanya katika Wilaya na Vikosi vyote hapa Mkoani Mwanza.
Amewataka askari kukomesha vitendo vya ubabaishaji kwa wananchi na ubambikaji kesi kama vipo, mfano kesi ya madai inabadilishwa kuwa kesi ya jinai jambo ambalo linanyima haki wananchi na kuchafua sifa nzuri ya Jeshi la Polisi.
Hivyo ubabaishaji wa aina hiyo
uepukwe na yeyote atakaye bainika anafanya hivyo hatua za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi yake.
Sambamba na hilo Kamanda Msangi amewataka askari wa kila kitengo kusimama vyema katika nafasi zao, ambapo alisema kila askari akiwa vizuri katika utendaji kazi hakutakuwa na malalamiko yeyote toka kwa wananchi hivyo ni jukumu la kila askari kuhakikisha dhamana aliyopewa na serikali ya kulinda wananchi pamoja na mali zao anaisimamia vizuri bila ubabaishaji wa aina yeyote ile.
Pia aliwataka askari wawe na
utaratibu mzuri wa upokeaji, utunzaji na uondoshaji wa vielelezo katika vituo
vya Polisi, kwani katika baadhi ya vituo vya Polisi lipo tatizo la utunzaji wa
vielelezo hivyo hataki kuona tatizo hilo linaendelea kuwepo. Vilelele aliwataka
Maofisa wa Polisi wa Wilayani hapo kuzingatia taratibu zilizowekwa kisheria za
uondoshaji wa vielelezo katika vituo vya Polisi.
Hata hivyo alisema hategemei kuona
mlundikano wa vielelezo katika vituo vya Polisi ambavyo vimekaa vituoni mwaka
mmoja au zaidi.
Kwani madhara yake vinaweza
kuharibika, kupoteza ubora au kupotea alafu baadae liwe deni kwa Jeshi. Hivyo
aliwataka askari kutekeleza maamuzi ya mahakama haraka juu ya uondoshaji wa
kielelezo/vielelezo baada ya kesi kumalizika mahakamani.
Kwa upande wa upelelezi alisema
kumekuwa na tatizo la kuchelewesha upelelezi wa kesi nyingi. Jambo ambalo
linawanyima wananchi haki. Hivyo alimtaka Mkuu wa Upelelezi Wilayani hapo
kushughulikia suala hilo mapema lisiwepo katika himaya yake ili haki ipatikane
haraka bila uonevu wa aina yeyote.
Pia aliwapongeza askari wa Wilaya
hiyo kwa utendaji mzuri wa kudhibiti uhalifu, aliwataka waongeze juhudi kwa
yale maeneo yenye vibaka na uhalifu mwingine mdogomdogo kwani anaamini
wanaweza. Ushirikiano ulipo na Viongozi wa ulinzi na usalama Wilaya, Wananchi
na vyombo vingine vya ulinzi na usalama udumishwe ili Sengerema iwe salama
zaidi kwani amani ikiwepo maendeleo yatapatikana zaidi
ASKARI ACHENI KUBAMBIKIZA WATU KESI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment