Jeshi la Polisi mkoani
Pwani limeanzisha kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva
wanaowashawishi askari kupokea rushwa pindi wanapokutwa na makosa ya usalama
barabarani na kuahidi kuwa litawapandisha vyeo askari watakamata dereva hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani Jonathan Shana, amewaambia waandishi wa habari kuwa huo ni mkakati mmoja
wapo wa kupambana na ajali za barabarani mkoani humo.
Aidha Kamanda Shana amefafanua kuwa
kikosi kazi hicho ambacho kinaundwa na makachero kimeshaanza kazi na hatua za
kisheria zitachukuliwa mara moja kwa madereva watakaokutwa na makosa hayo ikiwa
ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kamanda Shana amesema mkakati huo wa
kupunguza ajali pia utalenga kuwafungia leseni pia kutangaza kwenye vyombo vya
habari makampuni yote ya mabasi ambayo yatakuwa yamekithiri kwa makosa ya
mwendo kasi.
ASKARI WAAHIDIWA KUPANDISHWA VYEO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 02, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment