Wataalamu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingita katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi (Luwasa), wametakiwa
kufanya kazi mchana na usiku ili kubaini changamoto zilizopo kwenye
miundombinu na kuchukua hatua.
Agizo hilo llimetolewa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe alipokuwa akizungumza na watendaji wa mamlaka hiyo alipotembelea kuona maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Ng’apa uliopo kwenye manispaa hiyo.
Amesema ameridhishwa na jitihada zinazofanywa
na mkandarasi, huku akisikitishwa na kupasuka kwa mabomba wakati wa
kusafirishia maji kutoka chanzo hicho hadi kwenye matanki
Kamwelwe amesema wizara yake imetekeleza
miradi mbalimbali inayohusu maji ukiwemo wa Ruvu Juu na Chini katika Mkoa wa
Pwani, lakini hajawahi kuona mabomba yakipasuka hovyo kama yalivyokuwa kwenye
mradi huo wa Ng’apa
“Nimeshtuka kwa nini haya mabomba yanapasuka
mara kwa mara, hivyo ninawaagiza watalaamu kaeni hapa na mfanye kazi mchana na
usiku ili kuona shida ni nini?”amesema Kamwelwe.
Ameongeza kuwa kasoro zilizopo na mkandarasi
aweze kuzirekebisha kabla hajaondoka kuelekea nchini kwao India.
Kwa Waziri Kamwelwe ni ziara ya pili mkoani
Lindi ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja kukagua mradi huo, ambapo
alimuondoa Mkurugenzi wa Luwasa, Riziki Chambuso kwa kushindwa kuwajibika
ipasavyo na kumkaimisha Juma Sudi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani (Mtuwasa)
Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Shaibu Ndemanga
akimwakilisha Mkuu wa mkoa, Godfrey Zambi amesema ameanza kufarijika na
kazi mzuri inayofanywa na kikosi kazi cha kutoka Mtuwasa
Amesema tangu waziri afanye mabadiliko hayo
ya uongozi, baadhi ya maeneo kama vile Angaza na Mtanda wakazi wake wameanza
kupata huduma ya majisafi na salama kwa matumizi ya binadamu
Mradi wa maji Ng’apa ulikabidhiwa kwa
Kampuni ya Oia ya India mwaka 2013 na kazi hiyo ilitakiwa ikamilike Novemba
2015, lakini umekuwa ukisuasua utekelezaji wake na kusababisha wakurugenzi
watatu wa Luwasa kuondolewa kwa madai ya kushindwa kusimamia upatikanaji wa
huduma ya maji.
WAZIRI AAGIZA WATAALAMU WATAKIWA KUFANYA KAZI MCHANA NA USIKU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment