PICHA HAIHUSIANI NA TUKIO |
Watoto wanne
wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto walipokuwa wamelala
chumbani katika tukio lililotokea mtaa wa Geita Road Kata ya Nyatukala mjini
Sengerema.
Mkuu wa Wilaya
ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema tukio hilo lilitokea saa tano usiku wa
Februari 28, 2018 na kuwataja watoto hao kuwa ni Redia Elias (10), Modesta
Elias (9), Steven Deogratias (9), na Kizengela Elias mwenye umri wa miaka
ninane.
Amesema wakati
moto huo uliotokana na mshumaa kushika chandarua na kuunguza godoro walilokuwa
wamelalia, mama yao alikuwa amelala kwenye nyumba nyingine ya familia hiyo
“Watoto wote
ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Pambalu na wanatarajiwa kuzikwa kesho,” amesema
Kipole.
Mmoja wa
majirani wa familia hiyo, Amas Juma amewataka wazazi kuwa makini pale
wanapolazimika kuwawashia watoto mishumaa kwa kuhakikisha inazimwa kabla ya
kulala.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema polisi wanaendelea na uchunguzi
kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari watoto
wanapobaki wenyewe nyumbani.
WATOTO 4 WAFARIKI KWA KUTEKETEA KWA MOTO MWANZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment