Naibu Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Roma
Mkatoliki kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa kipindi cha miezi sita.
Akizungumza
leo Machi 1, 2018 na baadhi ya wasanii aliowaita na kuwaeleza dosari zilizopo
katika nyimbo zao, Shonza amesema baada ya Roma kupewa muda wa kufanya
marekebisho wimbo wake wa Kibamia ameshindwa kutekeleza agizo hilo
“Mpaka sasa hajaufanyia
marekebisho na wimbo huo unaendelea kurushwa kwenye vyombo mbalimbali vya
habari. Tulitoa muda kwa Roma kufanyia marekebisho wimbo wake tangu mwaka jana
mwishoni lakini mpaka leo ni miezi mitatu ameshindwa kutekeleza hilo,” amesema
Shonza.
Amesema jana
msanii huyo alipigiwa simu ili leo afike katika kikao hicho kwa ajili ya
kujitetea, pia hakutokea.
Roma Mkatoliki afungiwa kujihusisha na muziki kwa miezi sita
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment