Mbunge wa jimbo la
Singida Magharibi. Elibariki Kingu amefunguka kwamba yeye anakula bata (kufanya
starehe) lakini pia anakumbuka kufanya maendeleo kwa kutumia uwezo wake binafsi
ikiwa ni pamoja na wanachi na serikali kwenye jimbo lake.
Mh. Kingu amesema amesema maeneno
hayo huku ikidhaniwa kwamba anarusha dongo kwa mtu anayemsema kwamba hafanyi
kazi ambapo Mbunge huyo amesema kwamba "Najenga mashule mapya karibu
kila eneo kwa nguvu zangu, serikali yangu na wananchi, nanunua vifaa Tiba na
kuipa serikali zahanati zote kwa pesa ambayo walipaswa watumie wanangu".
Mbunge huyo amefafanua kupitia
Mtandao wake wa Instagram kwa kuweka majengo ya kituo cha afya cha Ihanja
ambapo amesema kuwa licha ya kituo hicho kuwa cha kisasa lakini pia kitakuwa na
uwezo wakufanya mpaka upasuaji mkubwa.
Kituo cha Afya cha Ihanja
kinachojengwa chini ya uongozi wa Mbunge Kingu
"Mjinga mmoja anakaa
kwenye 'keyboard' anasema eti mbunge ana kula bata bata nakula lakini ninajenga
zahanati kila kijiji jimboni kwa pesa zangu, serikali na wananchi,"
ameandika Mh. Kingu.
Mh. Kingu ameongeza "Nimesaidia
akina Mama mitaji pikipiki zaidi ya 50 mpaka sasa za milioni 90 nimegawa kwa
vijana kwa hela yangu. huyu mpuuzi akitaka ajue mapenzi ya hawa wananchi aje
aongee huu upumbavu wake kwa wapiga kura wangu kama hawajamchoma moto".
Mbunge Kingu asema anapenda starehe lakini anakumbuka kazi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment