Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amefunguka
na kudai baada ya kufanyiwa vipimo vyote nchini India amebainika kuwa na tatizo
kwenye fuvu lake la kichwa ambapo hilo ndio lililokuwa likimfanya akose
usingizi hapo awali bila ya yeye kujitambua.
Wastara ameeleza hayo mara
alipowasili katika ardhi ya Tanzania akiwa anatokea nchini India ambako alienda
kufanyiwa matibabu ya mguu pamoja na mgongo uliyokuwa unamsumbua kwa kipindi
kirefu lakini baada ya kufika huko alikutwa na matatizo mengine tofauti na
hayo.
"Ni tatizo ambalo lilikuwa
linahitajika kuchukuliwa umakini kwa sababu muda mwingi nilikuwa nalalamika kukosa
usingizi, kitu ambacho mimi mwanzo nilikuwa nadhani labda ni kutokana na mawazo
niliyokuwa nayo lakini siyo hivyo. Kwenye fuvu la kichwa kuna mpasuko kwa nje
na kusababisha kama uvimbe jambo ambalo lilikuwa linanisababishia kukosa
usingizi", amesema Wastara.
Pamoja na hayo, Wastara ameendelea
kwa kusema "nimefanikiwa kupata dawa pia na ninatakiwa nitumie
kila baada ya miezi mitatu na kama kuna uwezekano wa kupata matibabu hapa hapa
nchini itakuwa vizuri. Wenyewe wamenishauri kama itawezekana niweze kupata bima
ya afya kubwa kwa sababu kama kuna ulazima wa kurudi kila baada ya miezi mitatu
iwe rahisi ili niweze kuangalia tatizo la kichwa kwa sababu sio jambo la
kulifanyia masihara".
Kwa upande mwingine, Wastara amesema
anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kurudi salama nchini pamoja na
tatizo lake la mguu linaendelea vizuri japokuwa bado yupo kwenye uangalizi.
Nimeambiwa Nina mpasuko kwenye fuvu la kichwa - Wastara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment